Makao
makuu ya polisi wa kutuliza ghasaia yaliteketezwa kabisaBomu kubwa la
kutegwa ndani ya gari limelipuka kwenye makao makuu ya polisi wa
kutuliza ghasia mjini Cizre, kusini mashariki mwa Uturuki na kuwauwa
polisi 11, na wengine 70 wamejeruhiwa
Haijafahamika
ni nani aliyetekeleza shambulio hilo, lakini vyombo vya habari vya
Uturuki vimelaumu chama cha wafanyakazi wa kikurdi kilichopigwa marufuku
cha -PKK - kuhusika na shambulio hilo.
Wakazi wa
mji wa Cizr wamekuwa chini ya tahadhari ya kutotoka nje kwa miezi
kadhaa iliyotangazwa na mamlaka za Uturuki zinazopigana dhidi ya PKK.
Shrika la
Umoja wa Mataifa la haki za kibinadamu limedai uchunguzi ufanyike
kuhusu madai ya kwamba watu zaidi ya 100waliteketezwa kwa moto hadi kufa
walipokuwa wamewomba hifadhi kwenye chumba cha chini ya ardhi mjini
Cizre - mji wenye umskini uliopo mpakani na Syria.
Serikali ya Uturuki imepinga madai kwamba raia walilengwa na mashambulio hayo.
Vikosi
vya usalama vya Uturuki vimekua vikiendesha misururu ya mashambulio
dhidi ya PKK tangu kuvunjwa kwa mkataba wa miaka miwili wa usitishaji
mapigano wa mwezi Julai mwaka 2015.
tangu
wakati huo, harakati za kijeshi kusinini mashariki mwa nchi zimekuwa
zikiendelea PKK wakilipiza kisasi ambapo mamia ya watu wameuawa.
Mzozo wa
PKK nchini Uturuki unaonyesha ishara ya kusambaa kote nchini anasema
mwandishi wa BBC Mark Lowen, na serikali imekataa mashautriano yoyote
hadi pale kundi hilo litakaponyang'anywa silaha zote.
Ghasia za hivi punde zinatokea wakati jeshi la Uturuki likijihami vilivyo kufuatia jaribio la mapinduzi la mwezi Julai.
sambamba
na wapiganaji wa PKK, Uturuki inapigana na Islamic State, ambalo
wapiganaji wake waliendesha msururu wa mashambulio ya umwagaji damu
katika kipindi cha mwaka uliopita.
PKK,
ambacho kimepigwa marufuku nchini Uturuki , kilianza mashambulizi yake
mnamo mwaka 1984, kikidai kupinga mamlaka za Uturuki kuwabagua na
kuwatesa wakurdi. BBC
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )