Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Q Chief amesema alienda kushoot video ya wimbo wake mpya Afrika Kusini ili kupata kitu kizuri.
“Mashabiki wasione ukimya, kuna mambo mazuri soon yanakuja, videos pamoja na mambo mengi mapya,” alisema Q Chief. “Nimetoka Afrika Kusini hivi karibuni kwa ajili ya video yangu mpya, nimefanya na Justin Campos, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula,”
Pia mwimbaji huyo amewashukuru mashabiki wake pamoja na media kwa kuendelea kusupport muziki wake.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )