Kaimu
Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike
akimkabidhi funguo na nyaraka Bw. Thomas Kone (35) kwa ajili ya Bajaji
mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli baada ya kumuona katika TBC1 akiwa anatafuta msaada
wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto
wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na
ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi.
Bw. Thomas Kone akipanda kwenye bajaji aliyokabidhiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Naibu
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akisalimiana na Bw. Thomas Kone
alipokwenda Kumkabidhi Bajaji kwa Niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )