Featured
Loading...

Unaweza Kuongeza ’’Hisia na Nguvu za Kiume’’ kwa Kufanya Yafuatayo



TIP: Fanya mazoezi ya "aerobics" (mazoezi yanayotegemea kasi na kuimarisha afya ya moyo, mapafu, na mishipa ya damu)angalau mara tano (5) kwa wiki. Mazoezi haya ni pamoja na kukimbia, kutembe kwa haraka haraka, kuruka kamba kuogelea, kuendesha baiskeli na mengine mengi kama hayo. Pia hakikisha
unakula samaki wa baharini "sea food" kama vile pweza na wengineo kwa kiasi kikubwa.

KWA NINI: Mzunguko wa damu wa kutosha husaidia ubongo kufanya kazi vizuri hivyo kuwa na hisia nzuri. Halikadhalika, mzunguko wa damu ni muhimu sana kwa NGUVU ZA KIUME. Mazoezi huongeza kiwango cha kemikali ya asili itwayo Nitric Oxide (NO), ambayo husaidia mishipa ya damu kutanuka, hivyo kuwa na uwezo wa kupitisha damu nyingi. NGUVU ZA UUME hutokana na damu nyingi kwenda kwenye uume. Upungufu wa kemikali hii, huchangia sana katika tatizo la UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Halikadhalika vyakula ambavyo hupatikana baharini, kama vile samaki, huwa na kiasi kikubwa cha kirutubisho kinachoitwa "ARGININE". Arginine ndiyo hutumika kitengeneza kemikali ya Nitric oxide (NO), ambayo kama tulivyosema hao awali, kemikali hii husaidia mishipa ya damu kutanuka hivyo kuongezeka ukubwa na kupitisha damu nyingi zaidi. 
HITIMISHO: Inawezekana imani iliyosambaa mtaani kuhusu nguvu na kazi ya SUPU YA PWEZA ikawa na mashiko ya kisayansi.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top