Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mhandisi Steven Mlote(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,wakati wa alipokuwa akitoa tamko la baraza hilo juu ya kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati ya 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja ,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini,Katikati Kaimu wa baraza hilo Dkt. Adolf Rutayuga na Mkurugenzi wa Udhibiti,Ufuatiliaji na Tathimini Bi. Agness Ponera.
Baadhi ya
wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwa kwenye
mkutano wakati Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi Steven Mlote(hayupo
pichani)alipokuwa akiongea na waandishi habari jijini Dar es Salaam
kuhusiana na tamko la baraza hilo kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo
ambapo kati hivyo 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa
Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja,ikiwa katika jitihada za
kuboresha elimu ya ufundi nchini.
Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kuwa vyuo 5 vimefungwa
kuendesha mafunzo na kufutwa kwenye rejista ya vyuo vya ufundi
nchini.Pia Baraza limetangaza kuwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi
bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vimepewa muda wa wiki mbili na
kutakiwa vijisajili mara moja kwenye Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa
hatua kali za kisheria.
Vilevile,
vibali vya usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia
ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati vyuo 57
vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya
ithibati, imetangazwa jana.
Akiongea
katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza (NACTE),
Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa
vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti
ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini,
na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.
KUONA VYUO VILIVYOFUNGIWA BOFYA HAPA. (P.T)Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )