Donald Trump amekuwa akishutumiwa kwa kauli zake
Mgombea
urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesisitiza
kwamba hakuna mgawanyiko kwenye kambi yake ya kampeni, licha ya taarifa
kudokeza kwamba kuna mzozo mkubwa katika chama hicho.
Akihutubu katika mkutano wa hadhara Florida, Bw Trump amesema kampeni yake "inafanya vyema sana".
Vyombo
vya habari vya Marekani viliripoti kuwepo kwa mvutano baada ya Trump
kurejea matamshi yake ya kushambulia wazazi wa Mwanajeshi aliyeuawa
nchini Iraq.
"Ningetaka
kuwafahamisha tu kwamba kampeni inaendelea vyema sana," amewaambia watu
waliohudhuria mkutano wake eneo la Daytona Beach.
Awali,
msaidizi mkuu wake Donald Trump Paul Manaford alikuwa pia amekana
taarifa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa kwenye kampeni baada ya kile
kinachodaiwa mfululizo wa kauli za mgombea huyo wa chama cha Republican,
zenye kukwaza.
''Kampeni ziko vizuri, tumejipanga, tunasonga mbele,'' aliiambia kituo cha runinga cha Fox News.
Baadhi ya Maafisa wa Kampeni za Trump wamesema ''wanahisi kuwa wanapoteza muda wao''.
Hata hivyo, Manafort amemlaumu mpinzani wa Trump wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton kwa ripoti hizo
Bw
Manafort amesema watu wengi bado wana imani na Bw Trump''Hii ni kauli
nyingine ya Clinton ambayo imebebwa na vyombo vya habari, amesema
''Bwana Trump amejitokeza wiki hii kwenye mikusanyiko mikubwa sana ya
watu walifurika mpaka mtaani''.
Siku ya
Jumatano Bw Trump mwenyewe pia aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter
kuwa ''kuna umoja kwenye Kampeni yangu, pengine mkubwa zaidi kuliko siku
zote''.
Vita
vyake vya maneno na Khizr na Ghazala Khan, wazazi wa Kapteni Humayun
Khan aliyeuawa nchini Iraq, vimesababisha watu kutofautiana ndani ya
Chama cha Republican. BBC
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )