Baadhi
ya wakazi wa mkoa wa Kagera usiku wa saa tano kasoro September 11 2016
wametoneshwa kidonda baada ya tetemeko dogo kutokea ikiwa ni ndani ya
saa 48 baada ya tetemeko la kwanza lililoua watu 16.
Baada ya tetemeko la pili ambalo bado madhara yake hayajaripotiwa, reporter wa AyoTV
Bukoba amesema baadhi ya watu wametoa magodoro ili walale nje wakihofia
kutokea tena kwa tetemeko jingine usiku huu na likawakuta ndani ya
nyumba.
millardayo.com na AyoTV
zinaendelea kufatilia kwa ukaribu ili kukupa kila kinachoendelea ila
kwa sasa unaweza kumsikiliza Mtangazaji/Mwandishi wa Radio kutoka Bukoba
kwa kubonyeza play hapa chini.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )