Mkuu
wa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu akiongea na wananchi wa kata ya
Nkololo wilayani humo, wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo wilayani
humo 2016/17.Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga (Kulia) akikata utepe
kuashiria kuzinduliwa kwa msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17, (kulia)
ni Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya hiyo Duka Mashauri Mapya.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu kwa
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Bariadi Robert Rweyo (katikati)
pamoja na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Duka Mashauri
Mapya.Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu bure kwa
wananchi wa kata ya Nkololo, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Msimu wa
kilimo wilayani humo 2016/17.Wananchi wa kata ya Nkololo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga.( hayupo pichani).
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu
Festo Kiswaga jana alilazimika kunyeshewa mvua akiwahamasisha wananchi
wa wilaya hiyo kulima mazao kwa kitaalamu ikiwa pamoja na kugawa mbegu
bure kwa baadhi ya wananchi pamoja na viongozi.
Hali hiyo ilitokea katika kata na kijiji
cha Nkololo wakati Mkuu huyo wa wilaya alipokuwa akizindua msimu wa
kilimo wilayani humo 2016/17, ambapo sherehe hizo zilihudhuliwa na
viongozi wa halmashauri, madiwani pamoja na watendaji wote wakiwemo
wananchi.
Kiswaga alisema kuwa ofisi yake imejipanga
kuhakikisha wananchi wanalima na kupata mazao kwa kiwango kikubwa ili
kuweza kuondokana na janga la Njaa ikiwa pamoja na kuachana na utamaduni
wa kuomba chakula serikalini.
Alisema katika kuhakikisha suala hilo
linafanikiwa aliagiza kila kaya kuhakikisha inalima hekari nne za mazao
mbalimbai, huku kila hekari moja zao moja, ambapo aliyataja mazao
yatakayopewa kipaumbele kuwa ni Mahindi, Pamba, Mbaazi pamoja na
Choroko.
Alisema kila kaya itatakiwa kulima mazao
hayo katika msimu huu na misimu mingine mbeleni, kama hatua ya kuazia
katika mpango ambao alisema ameuanzisha Ushirikishwaji wa wananchi
katika kilimo kuondoa umaskini na Njaa.
Alisema katika mpango huo uhakika
umeonekana kuwa wananchi wa wilaya hiyo hawataomba chakula cha msaada
kutoka serikalini, ikiwa pamoja na kukuza uchumi wao na jamii kwa ujumla
kwa mazo ya biashara ambayo ni Mbaazi pamoja, Choroko pamoja na Pamba.
Aidha alisema kulima mazao hayo manne
itakuwa lazima, ambapo aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa haraka
ofisini kwake au kwa viongozi wengine kwa wafanyabiashara au makampuni
yatakayobainika kuuza na kusambaza mbegu na madawa feki.
” ninategemea wananchi wote mtaunga mkono
mpango wangu huu ambao tunaanza na mazao ya aina nne, niwatake toeni
taarifa kwa watu watakaowapatia mbegu na madawa feki, watalam wa
halmashauri lazima kusimamia mpango kwa wananchi ili kuweza kuzalisha
kwa kiwango kikubwa msimu huu” Alisema Kiswaga.
Awali akiongea Makamu Mwenyekiti wa
halmashauri ya Wilaya Bariadi Duka Mashauri Mapya, alisema kuwa wananchi
wa wilaya hiyo hasa wanaopakana na hifadhi ya Taifa Serengeti wamekuwa
wakipata kero kubwa kutoka kwa wanyama hasa tembo kwa kuaribu mazao yao.
Alimuomba Mkuu huyo wa wilaya katika
kutekeleza mpango huo suala la wanyama hao lazima kuangaliwa kwa kiwango
kikubwa ikiwa pamoja na kupambana na watu wanaosambaza mbegu na madawa
feki.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )