Mrisho Ngasaa wakati akitumikia timu yake ya zamani.
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa leo
anatarajiwa kuwa na kikao na Mwenyekiti wa klabu ya Fanja ya Oman,
Sheikh Saif Abdullah Al-Sumri.Ngassa alitua Oman Alhamisi kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho ambayo kama yatakwenda vizuri, atajiunga na timu hiyo inayocheza Ligi ya Mabingwa ya Asia.
“Unajua huku kuanzia Ijumaa ndiyo mapumziko, watu hawafanyi kazi. Sasa mimi nilifika Alhamisi, ila Jumapili ndiyo nitakuwa na mazungumzo na Rais wa Fanja.” Amesema Ngassa
Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei mwaka jana akisajiliwa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri kwa mkataba wa miaka minne.
Hata hivyo, kocha aliyemsajili baba huyo wa Farida (9) na Faria (7) alifukuzwa baada ya miezi miwili tu na sasa tayari yuko Mbeya City ya Tanzania.
Katika kipindi cha mwaka mmoja wa kuwa Free State, Ngassa alifanya kazi na makocha wanne akiwemo huyu wa sasa, Mfaransa Denis Lavagne aliyeanza kazi Juni mwaka huu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )