Kwa siku na nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Zanzibar walisema kuwa hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa katika mkutano wa kutoa shukrani baada ya uchaguzi uliopita, imejenga imani kubwa kwa maendeleo na wananchi sambamba na kukemea suala la ubaguzi miongoni mwa wananchi na viongozi.
Moja kati ya wakati wa Zanzibar waliweza kutoa maoni tofauti tofauti kuhusiana na hotuba hiyo.
“Rais Magufuli alizungumzia vizuri suala la amani, halafu vilevile bila amani usingeweza kuja kunihoji hapa kwa hiyo amani ndio kila kitu,” alisema mkazi mmoja wa Zanzibar.
“Kwanza nampongeza mheshimiwa rais kwasababu hotuba yake imetufanya sisi vijana tuamke na tufanye kazi na sio kukaa maskani kama unavyotuona hapa,” alisema kijana mmoja.
Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli alisisitiza zaidi suala la maendeleo.
“Tunataka maendeleo, na mimi niwaombe ndugu zangu watanzania wote, lengo letu kubwa liwe maendeleo kwa watanzania, maendeleo kwa wazanzibar, maendeleo kwa wapemba, tupeleke Tanzania yetu mbele,tupeleke Zanzibar yetu mbele, vyama tuweke pembeni,” alisema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )