Featured
Loading...

ZITTO Kabwe Afunguka Kuhusu Utafiti wa Twaweza Kuhusu Imani Waliyonayo Wananchi Kwa Rais Magufuli


Kura za Maoni zilizotolewa na TWAWEZA zinaibua maneno ambayo unashangaa kuyasikia kwa wasomi, wengine maprofesa. Kwangu mimi naona masuala 2 muhimu


  • Matokeo yanaonyesha IMANI kubwa ambayo wananchi wanayo kwa Rais Magufuli. Hata hivyo IMANI hiyo inakuja na wajibu mkubwa sana na Rais asitumie vibaya imani hiyo. Kiongozi mwenye busara hawezi kutumia imani hii kwa kukandamiza demokrasia na kukanyaga Katiba. 
  • Matokeo pia yanaonyesha kuwa Wabunge na Madiwani kwa kiasi kikubwa wana IMANI ya wananchi wao wanaowawakilisha. Huu ni wajibu na fursa kwa Wabunge wa Upinzani kuonyesha uongozi mahiri wenye kutoa majawabu ya changamoto za wananchi kwenye maeneo yanayoongozwa na Vyama vya Upinzani.


Tujifunze kukubali tusiyopenda kuyasikia. Wakati tunapambana vita adhimu sana dhidi ya Udikteta Mamboleo unaonyemelea nchi yetu, pia kwa nguvu hizo hizo tuonyeshe tofauti ya kiuongozi katika Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji tunayoongoza

By Zitto Kabwe

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top