Basi lenye namba za usajili T990 AQF mali ya kampuni ya Safari Njema
liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, jana liliteketea kwa Moto
maeneo ya Kimara Stop Over-Suka, mara baada ya kugongana na Lori
lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili
hazikujulikana mara moja).
Imeelezwa kuwa mali zote zilikuwemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa mtu mmoja amefariki Dunia katika ajali
hiyo na wengine 16 wamejeruhiwa na baadae kukimbizwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa matibabu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )