VERA
SIDIKA: Miongoni mwa wakenya maarufu wanao daiwa kutumia mafuta
ya mchekanambingu kwa ajili ya kungarisha nyota zao
*****
Mchungaji
Lewis Njoroge wa kanisa la New Tongue Faith lililopo jijini
Nairobi hapa Kenya, ameibuka na kujibu tuhuma zinazo mkabili za
kukutwa na mafuta ya MCHEKANAMBINGU.
Pastor
Njoroge ambae kwa muda mrefu sasa amekuwa akiwatahadharisha
waumini wake na wakenya kwa ujumla kuhusu kutotumia MAFUTA YA
MCHEKANAMBINGU kwa madai kuwa ni MAFUTA YA KUZIMU , wiki
iliyopita aliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini
Kenya, akidaiwa kujipata matatani baada ya Mafuta ya
MCHEKANAMBINGU kukutwa ofisini kwake.
Mara
kadhaa Pastor Njoroge maarufu kama Pastor Njoroo,. Amekuwa
akiwakemea waumini wake pamoja na wakenya kwa ujumla,
kutothubutu kutumia MAFUTA YA MCHEKANAMBINGU kwa sababu ni
mafuta kutoka kuzimu, yanayo tolewa na mganga wa jadi kutoka
Tanzania, ajulikanae kama mungu wa kabili, ambae kwa mujibu wa
PASTOR Njoroge , ni wakala wa kuzimu.
Pia
Pastor Njoroge amekuwa akiwatuhumu baadhi ya wachungaji, wasanii
wakubwa na wafanyabiashara maarufu kujihusisha na matumizi ya
mafuta ya mchekanambingu.
Aidha
Pastor Njoroge amewahi kunukuliwa akitoa shutuma zake kwa
baadhi ya magazeti ya Kenya, akivitumuhu ku wahamasisha vijana
kutumia mafuta ya mchekanambingu.
“
Sasa hivi, kila mtu akiwa maarufu na kupata mafanikio hapa
Kenya, magazeti yana muhusisha mtu huyo na mafuta ya
mchekanambingu. Matokeo yake sasa hivi kila kijana, anafikiri
hawezi kufanikiwa katika jambo lake bila kutumia mafuta ya
mchekanambingu “….
Pastor
Njoroge aliongeza kwa kusema kuwa mafuta ya mchekanambingu ni
mafuta kutoka kuzimu, na yoyote atake jipaka mafuta hayo
anakuwa amejiunganisha moja kwa moja na utawala wa kuzimu.
Mafanikio atakayo yapata yatakuwa ya muda mfupi tu na malipo
yake yatakuwa makubwa kuliko mafanikio aliyo yapata.
Wiki
mbili zilizopita vyombo mbalimbali vya habari nchini Kenya,
viliripoti kuhusu tuhuma za kukutwa kwa mafuta ya
mchekanambingu kwenye ofisi za Pastor Njoroge, jambo ambalo
lilizua mtafaruku mkubwa kati ya Pastor Njoroge na waumini wake.
Inaelezwa
kuwa, mmoja kati ya wazee wa kanisa la New Tongue Faith,
aliingia ofisini kwa Pastor Njoroge kwa ajili ya kuchukua
documents. Sasa wakati anapekua makabrasha katika ofisi hiyo
alishangaa kukuta kibox chenye vichupa vinne kikiwa sambamba na
karatasi yenye maelekezo ya jinsi ya kutumia mafuta ya
mchekanambingu.
Ikadaiwa
kuwa, baada ya kuulizwa kuhusu mafuta hayo yamefikaje ofisini
kwake, Pastor Njoroge hakuwa na majibu yenye kueleweka.
Suala hili lilifika kwa wazee na viongozi wa kanisa kwa ajili ya kulijadili na baadae likavuja kwa waumini.
Akifanya
mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Kenya, Pastor
Njoroge alisema “ Mafuta hayo yalipandikizwa ofisini kwake, kwa
lengo la kumchafulia jina lake “.
“
Ndugu mwandishi, vita vyetu si kwa jinsi ya mwili. Vita
tunavyopigana wakristo ni vya rohoni. Nina wapinzani wengi sana
ambao wanajaribu kunikwamisha, lakini ninasema watashindana lakini
hawatashinda “.
Tulimpigia
simu dokta mungu wa kabili kupitia namba yake 0744 000 473
ili atueleze kama anamfahamu Pastor Njoroge, alijibu kwa ufupi “
Simfahamu “
Mafuta
ya mchekanambingu, yamekuwa maarufu sana hapa nchini Kenya,
ambapo inasemekana kuwa yanatumika kwa kazi mbalimbali kama vile
kusafisha nyota, kusafisha mwili, kumkinga mtu dhidi ya maadui,
kuimarisha mahusiano ya kimapenzi, kuharakisha ndoa, kumvuta mpenzi,
kuwakinga watoto, kukuza biashara, uongozi nakadhalika, huku
wateja wake wakubwa wakitajwa kuwa wanasiasa wakubwa, viongozi,
wafanya biashara, wasanii wa muziki, nakadhalika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
