Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilioishia...
Hadi
kunapambazuka sikuweza kumuona nesi phidaya, hali ya hatari ikaanza
kunijia kichwani mwangu na kuhisi nesi phidaya anaweza kuwa amekutwa na
matatizo, mlango ukafunguliwa na wakaingia manesi wawili pamoja na
madaktari wale wawili.Wakaanza kufungua kitandana na kukishusha chini
kidogo hadi kikafikia usawa mzuri wa kuweza kusukumwa.Pasipo hata ya
kunisemesha wakaanza kunisukuma na kunipeleka nisipo pajua huku nyuso
zao zikiwa na tabasamu ambalo sikuliewewa nini maana yeke
Endelea...
Wakazidi
kukisukuma kitanda nilicho lalia hadi hadi tukafika kwenye maja ya
mlango ambao juu kuna maandishi ya kiharabu ambayo sikuweza kuyaelewa,
nesi mmoja akausukuma mlango na kufunguka, na wakaniingiza ndani nikiwa
juu ya kitanda changu, mwanga mwekundu wa taa ulioo ndani ya chumba
ukazidi kuniogoesha.Chumba kizime kimezungukwa na mashine mbalimbali
ambazo sikujua zinakazi gani.Daktari mmoja akachukua mashine yenye
kimviringo mbele, kisha akakiwasha na kuanza kuzunguka, akachukua moja
ya miwani kubwa ambayo ni nyeupe akaivaa na kuanza kucheka kitu kilichoo
zidi kuniogopesha zaidi.
Gafla
taa ya mwanga mweue ikawashwa na kuwafanya madaktari na manesi,
kustuka, macho yetu wote tukayaelekezea mlangoni na kumuona nesi phidaya
akiwa ameshika, bastola huku jasho jingi likiwa linamwagika usoni,
akaanza kuzungumza kwa kiarabu na taratibu madaktari wakanyoosha mikono
juu wakitetemeka, akazungumza neno lililo wafanya madaktari kuanza
kurudi nyuma kutoka kilio kitanda changu.
“eddy, wamekufanya chochote kibaya?”
“hapana”
“powa”
Nesi
phidaya akazungumza neno jengine lililowafanya madaktari na manesi
kulala chini, sakafuni huku mikono yao wakiwa wameiweka juu ya vichwa
vyao.Nesi phidaya akanifwata hadi kitandani na kuuitisha mkono wake
mmoja kwenye, mgongo wangu na kuniomba niwe kushuka chini, japo
ninajihisi maumivu ila nikajikaza kiume kwani kuendelea kukaa haoa
kutahatarisha maisha yangu.
“jikaze baba yangu”
Nesi
phidaya alizungumza huku akiendelea kunishusha kwenye kitanda,
akanisaidia kusimama vizuri, huku muhimili wangu wote wa kusimama
nikiutegemea kutoka kwake, nesi phidaya akawatazama watu madaktari walio
lala chini, akazungumza neno la ukali lililo wafanya madaktari na
manesi kuzidi kuzifunika sura zao chini pasipo kuzinyanyua
juu.Tukafanikiwa kotoka nje ya chumba walicho niingiza, nesi phidaya
akafunga mlango kwa nje na sote tukaanza kuondoka taratibu huku nesi
phidaya akiificha bastola yake na baadhi ya wahudumu wakabaki wakiwa
wanatushangaa.Tukatoka nje na kukuta gari aina ya taksi ikiwa
inatusubiria
“ahaaaa”
Nilitoa
mguno wa maumivu baada ya mguu wangu nilio vunjika kugongwa kwenye
mlango nilipokuwa ninajiaandaa kuingia ndani ya gari, siti ya nyuma
“pole eddy”
“asante”
Nesi
phidaya akanisaidia kuingia ndani ya gari na kufunga, kisha yeye
akaingia kwenye siti ya mbele kwa dereva na kumuongelesha dereva kiarabu
na akaliondoa gari lake kwa kasi.
“asante sana, nesi phidaya”
“usijali nipo kwa ajili yako, ila ningependa uniite phidaya tu na si nesi phidaya”
“sawa”
Nikaendelea
kujilaza kwenye siti ya nyuma ya taksi tuiyo ipanda, ila kuna mwanga
mkali wa taa ukawa unaingia kwenye gari letu, ikanilazima kunyanyua
kichwa changu kutazama nyuma, nikaona gari ndogo ikija kwa kasi sana,
“phidaya kuna watu wanatufwata nyu……”
Kabla
sijamalizia sentesi yangu nikastuka risasi ikipiga kwenye kioo cha
nyuma na kunifanya nirudi chini, na kulala kwenye siti yangu.Dereva
akaanza kulalamika, na phidaya akaanza kumuhimiza dereva kuongeza mwendo
kasi wa gari,risasi zipatazo nne zikaingia kwenye kioo cha nyuma cha
gari na kushangaa ragi ikiaanza kuyumba huku dereva akiwa ameulalia
mskani wake,
“shit dereva amepigwa risasi ya kichwa”
Phidaya
alizungumza kwa kuchanganyikiwa kiasi kwamba na mimi nikaanza
kuchanganyikiwa, risasi zikaendelea kumiminika ndani ya gari na kuzidi
kunichanganya
“mtoe huyo dereva”
Nilizungumza
kwa sauti ya juu, phdiaya akafanya kama nilivyo muagiza, akaufungua
mlango wa dereva na kumsukumia kwa nje, kisha akafunga mlango na kukaa
kwenye siti ya dereva
“nipe bastola yako”
Phidaya
akanirushia kwa nyuma bastola yake, nikauchukua mkanda wa siti wa siti
ya nyuma na kuanza kuuvuta nikijaribu kuukata ila
nikashindwa.Nikamtazama
“eddy unataka kufanyaje?”
“nataka kukata huu mkanda niufunge mguu wangu unavuta sana”
Phidaya
akafungua kwenye kisanduku kilichopo pembeni ya siti ya dereva, na
kuanza kutoa vituvitu, vilivyomo ndani ya kisanduku, akabahatika kupata
mkasi na kunikabithi.Nikauchukua mkasi na kuukata mkanda wa siti na
kuufunga mguu wangu ulio vunjika, maeneo ya mapajani, hadi nilipo
hakikisha kwamba nimeunguza misuli kuvuta, nikajilaza vizuri kwenye siti
na kutoa magazine ya bastola na kukuta ikiwa na risasi za kutosha.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )