Meneja ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na mchango wake wa
kuinua vipaji vya wanamuziki wachanga hadi kuwa maarufu, Saidi Fella
‘Mkubwa Fella’ amedai muziki wa taarab haujakufa kama baadhi ya watu
wanavyodai.
Mkurugenzi huyo wa Yamoto Band ambaye ameingia kwenye muziki wa
taarab kwa kuanzisha bendi ya ‘Yah TMK Taarab’ amedai hakuna ukweli
wowote kwamba muziki wa taarab umekufa.
“Mimi siamini kwamba muziki wa taarab umekufa, mashabiki wapo
wanazaliwa kila siku wanataka muziki mzuri,” Mkubwa Fella alikiambia
kipindi cha Jahazi ya Sham Shama ya ITV.
Fella amesema yeye pamoja na bendi yake hiyo wamejipanga kuleta ushindani mpya kwenye muziki wa bendi kwa kuachia kazi nzuri.
“Ukija kwenye Yah TMK Taarab utapata kila kitu, sasa hivi tupo chimbo
tunaanda kazi nzuri, kwa sababu ingawa tuna watu ambao wanamajina
makubwa au wana uwezo mkubwa lakini mashabiki hawataki majina, wanataka
kazi, kwahiyo sisi tumejipanga vizuri na tunakuja kutoa burudani kwa
sababu mashabiki wapo wengi wanataka kazi,” alisema Fella.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )