Featured
Loading...

Nay Bwanaa!! Eti Nayeye Kaamua Kutaja Wasanii Wake Watano Wanaomkuna..!!!

 
Rapa Nay wa Mitego ameweka wazi wasanii watano wakali wa hip hop ambao amekuwa akiwasikiliza na kuwakubali siku zote kutokana na kazi zao katika muziki wa hip hop Tanzania. 
Nay wa Mitego alisema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo na kusema msanii wa kwanza ambaye yeye anakumbali na kumuheshimu ni Mr 2 maarufu kama '2 Proud' kwani huyo ndiye aliyemfanya yeye kuanza kuimba na anatamani kuona anaendelea kufanya muziki siku zote kwani akiwa anasikiliza kazi zake mpaka leo huwa anafurahi.

Mbali na Mr 2, Nay wa Mitego alisema rappa wa pili anayemkubali ni Fareed Kubanda, wa tatu ni Mr Blue, wa nne ni Mwana FA na rappa watano ni Nay wa Mitego mwenyewe ambaye anajua mashabiki zake wanataka nini na kuwapa muziki mzuri siku zote. 

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top