GAMBIA:
Hatimaye Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia, Yahya Jammeh (pichani)
amekubali kung’atuka na kuondoka nchini humo, rais anayetambuliwa na
jamii ya kimataifa amesema.
Rais aliyeapishwa juzi kwenye Ubalozi wa
Gambia nchini Senegal, Adama Barrow ametangaza hayo kupitia ukurasa
wake wa Twitter, baada ya mazungumzo ya saa kadha yaliyonuiwa
kumshawishi Bw Jammeh kukubali matokeo ya uchaguzi. Mataifa ya Afrika
Magharibi yamewatuma wanajeshi Gambia na kutishia kumuondoa Jammeh
madarakani kwa nguvu.
Adama Barrow alivyoapishwa kuwa rais wa Gambia.
Bw Barrow amekuwa nchini Senegal kwa
takriban wiki moja. ambako aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika
ubalozi wa Gambia mjini Dakar mnamo Alhamisi.
Bw Jammeh alikuwa amepewa muda wa
kuondoka madarakani kufikia saa sita mchana la sivyo aondolewe kwa nguvu
na wanajeshi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambao taya
wameshaingia nchini humo baada ya muda wake wa kuongoza kukamilika
Jumatano ya juzi licha ya kufanikisha kulishawishi bunge lipitishe
makubaliano ya yeye kuendelea kuwa madarakani hadi Mei.
Amekuwa akishauriana na Rais wa Guinea
Alpha Conde na mwenzake wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz huku
wanajeshi wa Ecowas kutoka Senegal na nchi nyingine za Afrika Magharibi
waliingia nchini humo baada ya kuapishwa kwa Bw Barrow na walisema
hawakukumbana na upinzani wowote.
Imeripotiwa kwa sasa hali huenda ikawa
shwali baada ya rais huyo kukubali kung’atuka madarakani kwa amani ili
amuachie mpinzani wake Adama Barrow ambaye amekwisha apishwa..
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )