Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK aka ‘Fundi Mitambo’ ametangaza
ujio mpya wa tamasha kubwa la Diamonds Are Forever 2017 ambapo safari
hii litafanyikia katika uwanja wa Taifa.
Muimbaji huyo alifanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza nchini mwaka
2012 katika ukumbi wa Mlimani City show ambayo ilihudhuriwa na watu
wengi kwa kiingilio cha Tsh 50,000.
Sallam akizungumza live na mashabiki katika mtandao wa Istangam
(Insta Live) alisema show hiyo ipo kwenye maandalizi na itafanyika
uwanja wa Taifa.
“Mjiandae na Diamonds Are Forever 2017, Diamonds Are Forever 2017 is back,” Sallam aliwaambia mashabiki.
Meneja huyo alidai safari hii tamasha hilo litafanyika uwanja wa taifa ili kuwapa fursa watu wengi zaidi ya kuudhuria.
Hata hivyo hakuweka wazi ni lini au mwezi gani tamasha hilo litafanyika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )