Featured
Loading...

Mahakama Yaridhia Umeya wa Mtoto wa Marehemu Sitta Manispaa ya Kinondoni..!!!

 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtambua Benjamin Samweli Sita (pichani) kuwa meya wa Kinondoni. Hukumu hiyo imetolewa leo baada ya mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa pili Ukawa waliofungua kesi kupinga matokeo ya ushindi huo.
Itakumbukwa kuwa, siku ya uchaguzi huo, polisi waliwakamata baadhi ya viongozi na wajumbe wa UKAWA sambamba na ongezeko la wajumbe batili upande wa CCM.
CHADEMA na Ukawa walifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupinga ushindi Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta huku walalamikaji wakiwa ni Mustapha Muro (aliyekuwa mgombea Meya Manispaa ya Kinondoni) na Jumanne Amir Mbunju (aliyekuwa mgombea Naibu Meya wa Manispaa hiyo) wote wakiwakilisha na Wakili wa CHADEMA, John Malya.
Kesi iliyofunguliwa dhidi ya Afisa Utawala wa Manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Samweli Sita (aliyetangazwa kuwa Meya) na Manyama Mangaru (aliyetangazwa kuwa Naibu Meya).

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top