Ray na Chuchu.
UTATA mzito umeibuka kuhusiana na mtoto aliyezaliwa na msanii
wa filamu Bongo, Chuchu Hans ambapo mashabiki wengi wametaka kujua kama
mtoto huyo ni wa Vincent Kigosi ‘Ray’ au nani na kwa nini kuna usiri
mkubwa juu ya kuzaliwa kwa mtoto huyo?
Ishu ya mimba awali kulikuwa na usiri mkubwa sana kuhusiana na
ujauzito wa Chuchu ambapo mara kadhaa alipobanwa na mwandishi wetu
alikana kuwa na mimba huku Ray naye akidai hajui lolote kuhusiana na
ujauzito wa mpenzi wake huyo.
”Mimi sina ujauzito, watu wanasema tu na kama unataka kuhakikisha,
nitakuja hapo ofisini kwenu mnipige picha,” alisema Chuchu lakini kila
alipoombwa kuonana na mwandishi wetu alikuwa akichenga. Hata hivyo, kwa
kuwa ujauzito haujifichi baadaye ilikuja kubainika kuwa, Chuchu ana
mimba kubwa ya kujifungua wakati wowote.
Taarifa za kujifungua siku chache baadaye zilivuja taarifa kuwa,
Chuchu kajifungua mtoto wa kiume lakini cha ajabu bado wahusika hao
waliendelea kuwa wasiri na hata walipopigiwa simu kuulizwa,
walitofautiana kwenye majibu yao.
Msikie Ray mara baada ya Chuchu kudaiwa kujifungua, paparazi wetu
alimpigia simu Ray lakini katika hali ya kusha-ngaza, alionesha kutojua
lolote.
“Unanipa hongera ya nini? Mimi sina mtoto bwana, hizo habari naziona tu mitandaoni, msinichurie,” alisema Ray.
Chuchu akubali
Wakati Ray akisema hana mtoto, Chuchu alikiri kujifungua mtoto wa kiume huku akim-shukuru Mungu kwa kumzalia mpenzi wake salama.
Madai mazito
Hata hivyo, wakati kukiwa na taarifa tofauti kuhusiana na kujifungua
kwa Chuchu, mtu wa karibu wa mastaa hao aliyeomba jina lake lisiandikwe
gazetini alimwaga ubuyu akisema:
“Chuchu kajifungua ila inadaiwa mtoto si wa Ray na ndiyo maana
amekuwa mgumu sana kuzungumza. Sura ya mtoto inaonekana haipo kwa Ray
wala Chuchu, sasa katika mazingira hayo si unajua mwanaume lazima
ustuke.
“Maana unaweza kujishebedua kuwa mpenzi wako kakuzalia mtoto, kumbe
si wako. Kwa hiyo ishu ni je, mtoto huyo ni wa Ray au kuna baba mwingne,
nadhani Ray akijiridhisha kuwa ni damu yake, atafunguka.”
Kufuatia madai hayo kuwa mtoto si wa Ray, mwandishi wetu alizungumza
na Ray tena lakini safari hii alionesha kuna kitu anachokificha kwani
alitoa maneno ya kushangaza akisema:
“Mimi watu wananiambia Chuchu kajifungua mbona bado na aliyesema kuwa
mimi sijui kama mtoto ni wangu ni nani? Mbona watu wanatunga sana
maneno, unajua sio kila mtu anapenda kuweka wazi mambo yake jamani, haya
ni maisha yangu, muda wa kuongea ukifika nitasema.”
Chuchu naye ajikoroga
Kuhusiana na madai kuwa, mtoto aliyejifungua si wa Ray, Chuchu
alijikoroga katika kutoa maelezo kwani safari hii alikana kujifungua
akisema, eti muda huo alipokuwa akiongea na mwandishi wetu alikuwa
hospitalini akijisikilizia.
“Kwani Ray alishakana kuwa mtoto si wake? Mbona mimi sijajifungua
ndio kwanza nipo hospitali, kuhusu kuficha mimba mwanzo hatukutaka kwa
sababu ya mambo binafsi sasa ndio tumeamua kuweka wazi ujauzito na mtoto
akipatikana tutaweka wazi. Hapa nipo Muhimbili, natarajia mtoto lakini
bado.”
Kuna kitu kinafichwa
Kufuatia utata huo uliopo kuhusiana na mtoto huyo aliyezaliwa,
inaonekana wazi kuna kitu kinafichwa ambapo wapo wanaosema labda
wanatafuta kiki na wengine kusema huenda ni kweli kuna utata juu ya baba
wa mtoto.
NB
Kujifungua kwa mwanamke ni jambo la heri hivyo hakuna sababu ya
Chuchu na Ray kuendelea kulifungafunga na badala yake wawe wawazi ili
pongezi ziweze kuwamiminikia kwa wakati muafaka.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )