Daimond Platnumz
Alama 21 zinazodaiwa ni chale zinazopatikana mgongoni mwa
mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ zimezua mambo baada ya
juzikati picha yake kutupiwa mtandaoni ikizionesha kwa uwazi na kuibua
mjadala mzito.
Picha hiyo iliyotupiwa mtandaoni
ilimuonesha Diamond akiwa kwenye moja ya shoo alizofanya hivi karibuni
huku akizungushiwa eneo ambalo lilionekana kuwa na chale, jambo
lililowafanya wadau kibao wazijadili.
Mmoja wa mashabiki hao aliandika hivi:
“Duh! Huyu jamaa hakamatiki aisee, kwenye shoo zake ni nyomi, anang’ara
kimataifa, utajiri wake usiseme, au ndiyo tuseme hizi chale zake
alizochanjwa ndiyo sababu?
“Yaani kama ni hivyo na mimi aniambie tu kachanjwa wapi ili na mimi niende kwa huyo mganga wake.”
Daimond Platnumz
Mwingine akaandika hivi: “Acheni zenu, huyu Mond ana nyota yake tu, hizo chale inawezekana ilikuwa ni tiba ya kawaida.
Akizungumza mmoja wa wasanii anayefanya poa licha ya nyota yake kutong’ara sana, D-Malick alisema:
“Unajua nasikia tu kwamba huwa wasanii wakubwa wanaendaga kwa
wataalam ‘kutengenezwa’ ili washaini, niliona picha moja inaonesha
Diamond akiwa amechanjwa chale mgongoni, aisee kama ndizo zinamfanya awe
na mafanikio hayo makubwa ipo siku nitamfuata anielekeze na mimi
niende.”
jitihada za kumtafuta
Diamond kuzungumzia mjadala huu ulioibuka kuhusiana na chale zake
zikihusishwa na kung’ara kwake lakini hakuweza kupatikana mara moja.
Daimond Platnumz
Hata hivyo, siku za nyuma Diamond
aliwahi kuongea na kusema kwamba, madai kuwa kufanya
kwake vizuri kwenye muziki kunatokana na mambo ya kishirikina siyo kweli
bali juhudi binafsi ndizo zilizomfikisha mahali alipo.
“Mafanikio yangu hayatokani na mambo ya
kishirikina, juhudi na maarifa ndiyo siri ya mafanikio yangu,” aliwahi
kusema hivyo Diamond.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )