Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Baada ya kuibuka msanii
chipukizi wa Bongo Fleva anayefanana sana kwa sura na msanii kutoka WCB,
Harmonize kiasi cha kubatizwa jina la ‘Pacha wa Harmonize’, Harmorapa,
katika mitandao ya kijamii inasambaa picha ikimuonesha pacha wa msanii
wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay Wa Mitego’, aliyebandikwa jina
la ‘Ney wa Mitego Rapa’.
Picha ya utani mtandaoni iliyofananishwa na Ney wa Mitego (kushoto) na (kulia) ni Emmanuel Elibariki ‘Nay Wa Mitego.
Mashabiki wa Ney wa Mitego hawajapendezwa na picha ya pacha wa Ney wa
Mitego, japo ni utani mashabiki hao wamedai inamdhalilisha Ney true
boy.
Mpaka muda huu Ney wa Mitego hajatoa tamko lolote juu ya picha hiyo ya pacha wake mtandaoni.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )