Featured
Loading...

Alikiba awapa zawadi mashabiki Kwa Kuachia Video Mpya.....Itazame Hapa

Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' Alikiba ameamua kuachia video ya wimbo wake wa zamani ambao ulivuja kama zawadi kwa mashabiki wake katika siku yake ya kuzaliwa.

Alikiba ambaye jana alikuwa anasherehekea kumbukumbu ya mwaka wa kuzaliwa aliamua kuachia video ya wimbo wa 'Maumivu Per Day' kama njia ya kusherekea siku hiyo na mashabiki zake.

"Nashukuru sana watu ambao wamenitakia kheri katika siku yangu ya kuzaliwa, nimejaliwa, kupendelewa na kupendwa pia nashukuru sana kwa jambo hilo, nawapenda wote na nitafanya kazi kwa nguvu zote kuwafanya mjivunie uwepo wangu. 

"Maumivu Per Day ni kati ya nyimbo zangu za zamani zinazopendwa nimeamua kuitoa japo siyo rasmi ili kusherehekea kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa na mashabiki zangu" alisema Alikiba.

watch here==>>> 

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top