Chadema
wamewataka wapiga kura kukaa umbali wa mita 100 wakati wa kusubiri
matokeo yao kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyia kesho katika
kata 42 nchini, ili kulinda kura zao.
Katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Jeshi la Polisi lilipinga wapiga kura
kukaa umbali wa mita 100 na baadaye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
kuhitimisha sakata hilo kwa kutamka kuwa kukaa umbali wa mita 200, baada
ya kupiga kura hairuhusiwi.
Akielezea
mwenendo wa uchaguzi huo, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa
Chadema, Benson Kigaila amesema sheria inaruhusu wapiga kura kukaa
umbali huo ili kulinda kura zao.
“Sheria
ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 inataka wapiga kura kusimama umbali wa
mita 100, kwa hiyo tuwaambie wapiga kura wetu wakishamaliza kupiga kura
wakae umbali wa mita hizo, waongeze na nyingine moja walinde kura zao,”
amesema
Kigaila
amewataka wapiga kura hao kwenda kwenye vituo vya kupigia kura na
kutimiza wajibu wao bila kuogopa kitisho chochote na baadaye walinde
kura zao hadi zitakapotangazwa.
“Waende
wakapige kura wasiogope kitisho chochote,” amesema na kuwataka baadaye
waende kwenye makao makuu ya kata yatakako tangazwa matokeo hayo
kuhakikisha, washindi wanatangazwa kwa haki.
Kiongozi
huyo wa Chadema amesema kumekuwa matukio ya uvunjaji wa haki kwenye
mikutano yao ya kampeni ikiwamo makada wake kuvamiwa na kupigwa.
“Upinzani
ukishinda utatangazwa wapende wasipende, ambaye atatangaza matokeo
tofauti ashughulikiwe kama mwizi mwingine wa kawaida kwa sababu wezi
huwa wanashughulikiwa,”
“Kwa
hiyo watu waende walinde haki yao ya kikatiba, wapige kura na walinde
matokeo. Yatangazwe matokeo sahihi.” amesema kiongozi huyo wa Chadema
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )