![](https://matukiotz.co.tz/wp-content/uploads/2017/11/21042004_1154909914609752_4307428894501240832_n.jpg)
Kutokana na kifo cha Ndikumana, Uwoya
alilazimika kwenda Rwanda kuhani msiba akiwa na mwanaye aliyezaa na
jamaa huyo, Krish, mama na baba yake na mabaunsa wa kumpa ulinzi. Chanzo
hicho kilieleza kwamba, watu mbalimbali nchini humo walikuwa na hasira
juu ya Uwoya kwamba ndiye aliyesababisha kifo cha Ndikumana kwani
alikuwa na msongo wa mawazo akimfikiria yeye kwa kuwa alimpenda na
kutaka wairudishe ndoa yao, lakini mwanamama huyo akawa anang’ang’ania
apewe talaka ambayo hadi Ndikumana anafariki dunia alikuwa hajaitoa.
Staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya. “Mashabiki wa Ndikumana walitaka
kumfanyia fujo Uwoya kwa kuwa wanadai ndiye chanzo cha kifo cha mpendwa
wao, lakini familia iliwazuia wasifanye hivyo kwa kuwa walishamsamehe
Uwoya ndipo hali ya amani ikawepo,” kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea kueleza kuwa, Uwoya
aliwasili nchini Rwanda Ijumaa iliyopita kwenda kuona kaburi la mumewe
ambaye alizikwa Jumatano iliyopita ambapo alipokelewa vizuri na mama wa
Ndikumana pamoja na familia kwa jumla. “Zile tofauti waliziweka pembeni
na mama Ndikumana akamwambia wamemsamehe hivyo ikawa ni kuomboleza upya
kwani Uwoya na mama’ke alikuwa akilia sana hadi kushindwa kutembea,”
kilisema chanzo hicho. Hata hivyo, alisaidiwa kwa kushikwa mkono na
wenyeji kwani mama huyo alikuwa akimpenda sana mkwewe Ndikumana kama
mtoto wake.
Baada ya chanzo kutiririka, Ijumaa
Wikienda lilimtafuta Uwoya ambaye alikiri kupokelewa vizuri na familia
pamoja na mama Ndiku ambaye alipomuona tu alimkumbatia huku akilia kwa
uchungu akimuita ‘mwanangu’. Naye msanii wa filamu, Michael Sangu ‘Mike’
ambaye ni mmoja wa watu waliosafiri alikiri kuwa walipokelewa vizuri na
hakuna tofauti yoyote iliyojitokeza. “Uwoya, baba, mama na Krish
walitangulia na ndege na walipokelewa vizuri kabisa na hakuna mtu
aliyewafanyia fujo wala nini, familia imewapokea kwa ukarimu na sisi
ambao tulifika baadaye maana tulisafiri kwa basi tulipokelewa vizuri
sana,” alisema Mike Sangu.
CREDIT: GPL
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )