Mwimbaji mpya wa Bongofleva Lulu Diva ambae mwaka huu umekua mwaka wake wa kwanza kupanda kwenye jukwaa la Tamasha la FIESTA, ameiambia Amplifaya ya CloudsFM kwamba amepewa taarifa za kuondolewa kwenye orodha ya Dar es salaam.
Mwanzoni
alikuwepo kwenye orodha ya watakao-perform Jumamosi November 25 lakini
kutokana na tamko la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kutoruhusu muziki kupigwa
maeneo ya wazi Dsm kuanzia saa sita usiku na kuendelea, Lulu amesema
jina lake limekatwa katika orodha hiyo na kurudishwa kwake ni iwapo FIESTAitaongezwa muda.
Lulu
alisema imefanyika hivyo sababu orodha iliyoandaliwa awali ilipangwa
kama ilivyopangwa kwenye mikoa mingine mwaka huu ambako tamasha hilo
lilifanyika mpaka alfajiri na ndio maana amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Paul Makonda asaidie ili FIESTA ifanyike mpaka asubuhi.
“Mwaka
huu ndio mwaka niliotimiza ndoto yangu na kutumbuiza kwa mara ya kwanza
kwenye FIESTA, ujira wangu ninaopata pale ninagawana na kila mtu alie
nyuma yangu, Dereva, Makeup Artist, Dancers wangu na wengine ndio maana
namuomba Mkuu wa Mkoa Makonda na Serikali kutufikiria tena sisi Wasanii”
– Lulu Diva
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )