Betty Mbereko na mwanaye, Farai Mbereko.
BETTY MBEREKO (40) mwanamke anayeishi Mwenezi huko Masvingo, Zimbabwe, ameolewa na mwanaye wa kumzaa aitwaye Farai Mbereko mwenye umri wa miaka 23.Katika hali hiyo ambayo ilitokea mwanzoni mwa mwezi huu wa Oktoba, mama huyo anategemea kupata mwanaye ambaye pia ni mjukuu wake. Mwanamke huyo amekuwa mjane kwa miaka 12 iliyopita ambapo amekuwa akiishi na mwanaye huyo.

Alithibitisha hivi karibuni kuwa ana
ujauzito wa miezi sita na hivyo akaona afadhali “aolewe” na mwanaye
kwani hakutaka kuolewa na mmoja wa wadogo wa marehemu mumewe, aliosema
wanamtamani.Betty aliishangaza mahakama ya kijijini kwake aliposema
alianza kuzini na mwanaye miaka mitatu iliyopita. Alisema baada ya
kutumia fedha nyingi kumsomesha Farai baada ya kifo cha mumewe, aliona
ana haki ya kufaidi fedha ya mwanaye na si mwanamke mwingine.
Tazama, nilihangaika kumsomesha
mwanangu na hakuna aliyenisaidia. Sasa mwanangu anafanya kazi na watu
wanasema nimefanya kosa. Acha nifaidi mazao ya jasho langu,” aliiambia
mahakama hiyo.Farai alisema yuko tayari kumwoa mama yake na atalipa
mahari kwa babu na bibi zake, ambayo baba yake hakuimalizia.Nafahamu
baba alikufa kabla ya kumalizia mahari; niko tayari kuilipa Ni yema
kutangaza kinachotokea kwani watu lazima wafahamu kwamba ni mimi nilimpa
ujauzito, bila hivyo watasema ni mzinifu,” alisema Farai.
Lakini kiongozi wa kijiji hicho,
Nathan Muputirwa, anasema: “Hatuwezi kuruhusu hili litokee kijijini
kwetu, kwani hii ni dalili mbaya. Hapo zamani watu hawa walistahili
kuuawa lakini leo hii hatuwezi kwa sababu tunaogopa polisi.”
Aliwaonya wawili hao wavunje ndoa yao au waondoke kwenye kijiji hicho ambapo walichagua uamuzi wa pili, na tangu hapo wameondoka kijijini hapo.
Aliwaonya wawili hao wavunje ndoa yao au waondoke kwenye kijiji hicho ambapo walichagua uamuzi wa pili, na tangu hapo wameondoka kijijini hapo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )