Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
jana amemkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho aliyekuwa Mbunge wa
Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, Jijini Mwanza katika uwanja wa Shule
ya Msingi Mhandu kwenye kampeni ya kumnadi mgombea udiwani Godfrey
Mahame.
"Nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii
ya leo ili nipate fursa ya kupigania mageuzi ya kisiasa na ya kiuchumi
Tanzania," amesema Nyalandu baada ya kukabidhiwa kadi.
Amesema ana shauku, furaha na heshima
kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa Chadema. Nyalandu ameongeza kuwa
katika majira na nyakati ambazo Taifa linapitia, mabadiliko ya kisiasa
nchini Tanzania ni lazima.
"Naungana na chama hiki pendwa ili
tutembee pamoja mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji tuwaambie wananchi
wakati wa ukombozi ni sasa," alisema Nyalandu.
"Saa ya mabadiliko imefika kwa mtu yeyote miongoni mwetu, tumepewa utayari wa kubadilisha mwelekeo wa nchi," amesema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )