Featured
Loading...

PATRICE EVRA AKUMBANA NA RUNGU LA FIFA NI BAADA YA KUMPIGA SHABIKI


Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya UEFA jana Ijumaa ya November 10 2017 limetangaza kumuadhibu beki wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anayeichezea Olympique Marseille ya Ufaransa kabla ya mkataba wake kuvunjwa, Patrice Evra kwa kosa la kumpiga shabiki wao wakiwa Ureno katika mchezo wa Europa League.

UEFA wamefikia maamuzi hayo kutokana na kitendo cha Patrice  Evra kumpiga teke shabiki wa Marseille ambaye walipishana maneno wakati wachezaji wa Marseille akiwemo Evra wakifanya warm up kuelekea kuanza kwa mchezo wao dhidi Vitoria.

Kufuatia kosa hilo UEFA sasa limemfungia Patrice Evra kutocheza mashindano yoyote ya UEFA hadi mwezi June 2018, taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya Marseillekuvunja mkataba na Evra kutokana na kufanya kosa hilo la kumpiga shabiki.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top