Mahakama
ya Rufaa Tanzania imekubali maombi ya Bodi ya Wadhamini ya Chama cha
Wananchi (CUF) inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho,Maalim Seif
Sharif Hamad katika shauri Namba 43/01/2017 kuhusu kumkataa Jaji Kihiyo
kusikiliza shauri la msingi.
Taarifa
hiyo ya maamuzi ya mahakama ya Rufaa, imetolewa mapema leo Disemba 22,
2017 kwa vyombo vya habari na Naibu Mkurugenzi wa Habari CUF, Mbarala
Maharagande.
“Mahakama
ya Rufaa imeipa ushindi Maombi ya Bodi ya Wadhamini ya CUF chini ya
Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad katika shauri Namba 43/01/2017
(From Civil Application No.23/2017) kuhusu kumkataa Jaji Kihiyo
kusikiliza shauri la msingi tajwa hapo juu.
“Shauri
hili ndilo linalohoji uhalali na mamlaka ya Msajili wa vyama vya siasa
nchini Jaji Francis Mutungi kumrejesha Lipumba katika nafasi ya Uongozi
ndani ya CUF baada ya kujiuzulu na kukubaliwa kujiuzulu kwake na Mkutano
Mkuu wa Taifa wa CUF uliofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo
Plaza Tarehe 21 August, 2017,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa, Jaji wa Mahakama ya Rufaa , Jaji Musa Kipenka
amekubaliana na hoja za Mawakili Wasomi wa CUF Halfani Daimu, Juma
Nassoro na Hashimu Mziray walizozitoa Mbele ya Mahakama hiyo.
Maharagande
amesema, maamuzi hayo yanaipa nafasi mahakama kuu kuendelea kusikiliza
shauri hilo ambalo Msajili wa Mahakama Kuu ameshalipangia jalada ambalo
linasikilizwa mbele ya Jaji Wilfred Ndyansobera.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )