Msanii
wa muziki wa Bongo Flava, Dudu Baya ameitaka serikali kupitia Baraza la
Sanaa Taifa (BASATA) kuwachukulia hatua wasanii wote ambao wameenda
kinyume na maadali kwa mwaka 2017 ili mambo hayo yasije kujirudia mwaka
2018.
Dudu
Baya akizungumza na E-Newz ya EATV amesema baadhi ya wasanii kwa mwaka
huu wameitumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuweka picha zisizo na
maadili kitu ambacho kimefanya jambo hilo kujadiliwa kuliko muziki wao.
“Watu
kama kina Nuh Mziwanda wanapiga picha za uchi uko na Shilole kipindi
kile uko bafuni unaoga kuna aja gani kuonyesha mashabiki wako, kuna mtu
gani asiyeoga hapa duniani. Ukija kama suala la mdogo wangu Young Dee
namkubali sana lakini alipiga picha na Amber Lulu za kumshika makalio,
huo ni ujinga,” amesema Dudu Baya.
Dudu
Baya ameendelea kwa kusema wasanii watumie mitandao kwa manufaa ya
kibiashara na endapo wakishindwa basi sheria ichukue mkondo wake.
“Nabahatika
nakutana na Amber Lulu au Gigy Money namwambia ebu kaza kwenye kipaji
chako ebu achana na upuuzi, sasa hivi mabinti wanaotaka kuingia kwenye
movie au muziki wasije kwa njia walizopitia Amber Lulu na Gigy,”
amesema.
“Kama
2017 yamefanyika sana, ni serikali au Basata kuja na tamko, hao ni watu
wa kutolea tamko atakayeenda kinyume basi sheria ifuate mkondo wake,
siyo wakati wakuonyana ni wakati wa tamko kabla ya kuingia 2018,”
amesisitiza.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )