Diwani
wa Chadema wa Donyomurwak wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, Lwite
Ndossi maarufu Nsonuu amejivua uanachama wa chama hicho.
Pia, amejiuzuru udiwani na ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa
iliyotolewa na idara ya itikadi na uenezi ya CCM Jumanne Desemba
19,2017 imesema Ndossi ameeleza sababu za kujiunga na CCM ni kuwa
kujiunga na watu wanaofanya siasa za kufanya kazi za maendeleo na si
kulumbana na maneno matupu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )