Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia
wizara ya Nishati, ametoa kiasi cha shilingi bilioni 210 kwaajili ya
ujenzi wa mradi mkubwa wa Umeme unaojengwa mkoani Ruvuma.
Akiongea
katika ziara yake ya siku tatu mkoani Ruvuma Waziri wa Nishati Dkt.
Medard Kalemani amesema Rais Magufuli ametoa fedha hizo kwa kushirikiana
na wahisani wengine.
“Mheshimiwa
Rais ndio ametoa fedha hizi bilioni 210 kwa kushirikiana na wahisani
ambapo bilioni 104 ni kwaajili ya kusambaza umeme katika wilaya zote za
mikoa ya Ruvuma na Songea”, amesema Waziri Kalemani.
Mradi
huo wa umeme unatarajiwa kuwafikia wananchi zaidi ya 32,000 katika
vijiji 120 vya mikoa hiyo. Waziri ameongeza kuwa mradi huo utawawezesha
wananchi kuingiza fedha nyingi kutokana na fursa zitakazojitokeza baada
ya kukamilika.
Kalemani
amewataka Wakandarasi kumaliza kwa wakati mradi huo kwani tayari
wameshapewa fedha zao bila kucheleweshewa. Mradi unatarajiwa kukamilika
mwezi Agosti 2018.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )