Mwenyekiti
wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda amepiga goti na
kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli aweze kukisaidia chama chake cha
Ada Tadea milioni 60 ili waweze kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge
unaotegemewa kufanyika mapema 2018
Shibuda
ameomba hilo leo Disemba 18, 2017 akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) na kusema endapo Rais akiwasaidia milioni 20 kwa
kila jimbo hivyo wataweza kushiriki uchaguzi wa marudio wa Ubunge katika
majimbo matatu ambao unategemewa kufanyika Januari 13, 2018.
"Nakuomba
utombee kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli atutazame tupate
ruzuku vyama visivyo pata ruzuku ili tuwe sawa na wale unaowapa ruzuku
lakini hawapendi kushiriki katika masuala ya uzalendo na utaifa, lakini
chonde chonde nakuomba utuombee" alisema Shibuda
Baada
ya maombi yake hayo Rais Magufuli alimuuliza kama yeye na chama chake
atashiriki katika uchaguzi wa marudio wa wabunge ndipo hapo aliporudi na
kuomba apewe milioni 20 kwa kila jimbo.
"Naomba
nisaidie milioni 20 kwa kila jimbo ili niwezeshe kwenda kugombea kwa
hiyo kwa majimbo matatu tusaidie chama milioni 60 kwa sababu
unaowapatika ruzuku hawatakwenda kushiriki" alisisitiza Shibuda.
Baadhi
ya Vyama vya siasa vya upinzani nchini Tanzania kikiwepo CHADEMA, CUF,
TLP, CHAUMMA pamoja na ACT Wazalendo vimejitoa kushiriki katika uchaguzi
mdogo wa marudio wa nafasi ya Ubunge ambao unategemewa kufanyika
Januari 13, 2018 kwa kile walichodai kuwa uchaguzi wa madiwani
uliofanyika karibuni haukuwa wa haki na ulitawaliwa na uvunjwaji wa haki
za binadamu na kanuni za uchaguzi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )