Mwanadada
Mange Kimambi ameibukia sakata la Wema Sepetu kurudi CCM,ikiwa ni siku
kadhaa zimepita tangu atabiri mpango wa Wema Kurudi CCM.
Akizungumza
kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Kimambi amesema Wema
hajawaangusha watanzania pekee bali amejiangusha yeye mwenyewe kwa
kutokua na msimamo.
“Hujawaangusha
waTZ tu, umejiangusha mwenyewe pia, your fans and everyone who cared
for you. Hivi kizazi hiki kina Winnie Mandela hakuna kabisa eehe?
Nakuonea huruma mnoooo sababu umepoteza credibly yooooote kwenye jamii”Ameandikia Mange Kimambi.
Hivi
karibuni Mange alisema kuwa anazo taarifa za uhakika kuwa Wema Sepetu
pamoja na Mama yake watarudi chama cha Mapinduzi akidai kuwa mama yake
amekubali kurudi isipokuwa anasuburiwa yeye.
Mange
alisema mpango wa kurudi CCM unafuatia Wema na Mama yake kubanwa katika
mambo mbalimbali kutokana na kuwa upande wa upinzani.
Wakati akitangaza kurudi CCM jana Wema alisema..
“Siwezi
Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is
everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani” .
Wema Sepetu.
Wema alijiunga chama cha Chadema mwezi februari mwaka huu akitokea chama cha Mapinduzi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )