WAKATI
uongozi wa Yanga hivi sasa ukiwa katika harakati zake za kuhakikisha
unakiimarisha kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri katika mechi zake
za Ligi Kuu Bara msimu huu zilizobakia, mshambuliaji wa timu hiyo,
Ibrahim Ajibu amezua hofu kubwa klabuni hapo.
Uongozi wa timu hiyo
umeingiwa na hofu kubwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa meneja wa
timu hiyo, Hafidhi Saleh kuwa Ajibu hatakuwepo katika kikosi cha timu
hiyo kitakachocheza dhidi ya Mbao FC.
Ajibu ataukosa mchezo huo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.
Ajibu ambaye pia
mpaka sasa ameshazifumania nyavu mara tano, kadi yake ya kwanza aliipata
katika mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini
Bukoba, kadi ya pili ni katika mchezo dhidi ya Simba na ya tatu ni dhidi
ya Prisons.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja
wa Yanga, Hafidhi Saleh, alisema: “Benchi letu la ufundi linaangalia ni
mchezaji gani atakayeziba nafasi yake katika mechi hiyo ambayo
tutacheza mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Chalenji.”
Sweetbert Lukonge, Dar es SalaamTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )