Mkurugenzi
wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi ameteuliwa
kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Nehemia Mchechu aliyesimamishwa
kupisha uchunguzi.
Mchechu
alisimamishwa kazi Desemba 16,2017 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi
yake ambazo hazijawekwa wazi wala mamlaka inayochunguza.
Akizungumza
jana Jumanne Desemba 19,2017 kuhusu mikakati yake baada ya kuteuliwa
na Bodi ya NHC kukaimu nafasi hiyo Maagi alisema, ‘’Kwa sasa siwezi
kusema kitu kwa kuwa hata ofisi bado sijakabidhiwa.”
“Nikikabidhiwa na nikiingia ofisini nitakuwa na cha kuzungumza lakini kwa sasa sina cha kusema,” alisema.
Maagi
ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili katika usimamizi wa biashara (MBA) ya
Chuo Kikuu cha Esami nchini Uganda na ni mhasibu anayetambulika na Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )