Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu yaDar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kesi
ya Dk Louis Shika hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba tatu za
mfanyabiashara maarufu Said Lugumi alizoahidi kuzinunua zote zipo.
Novemba
9, 2017 kampuni ya udalali ya Yono kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa nyumba mbili za Lugumi zilizoko
Mbweni JKT na moja Upanga jijini Dar es Salaam ambazo zote Dk Shika
alifikia bei ya kuzinunua kwa Sh3.2 bilioni.
Mambosasa
akizungumza leo Jumatano, amesema kesi yake haina mashiko hivyo
hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba hizo zipo na hajatia hasara .
Amesema
Dk Shika alikuwa akitamba kuwa ana fedha kumbe uwezo wake ni mdogo na
kusababisha kushindwa kulipa asilimia 25 kwa kila nyumba hizo.
‘‘Dk
Shika ni wa kumuonea huruma hana kitu tulisema tunamchunguza na
tutampeleka mahakamani lakini tumeona kesi yake haina mashiko ndiyo
maana hatuendelei nayo,” amesema Mambosasa.
Jeshi
la polisi kanda hiyo lilimshikilia na kumwachia kwa dhamana Dk Shika
ambaye alikuwa akituhumiwa kwa kuharibu mnada baada ya kushindwa kulipa
asilimia 25 ya fedha hizo ambapo nyumba za Mbweni JKT alifika bei kwa
Sh900 milioni na nyingine Sh1.1 bilioni, huku ya Upanga alifika bei ya
Sh1.2 bilioni
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )