Rais
mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amemtembelea mbunge wa
Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi
nchini Kenya.
Rais
Mwinyi akiambatana na mke wake na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini
Kenya, wamemtembelea Lissu hospitalini hapo alipolazwa tangu Septemba
7 anakotibiwa baada ya kuuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi
zaidi ya 30 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.
Rais
Mwinyi anakuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali waliomtembelea
Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambaye
hivi karibuni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan naye alifika
hospitalini hapo kumjulia hali.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )