Waziri
Mkuu wa mstaafu, Frederick Sumaye amesema zuio la kufanya mikutano ya
hadhara hadi mwaka 2020, linaminya uhuru wa wananchi wenye nia ya
kuanzisha vyama vipya ya siasa.
Sumaye
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati
Kuu ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini ametoa kauli hiyo jana
Januari 14, 2018 katika mahojiano na kituo cha Televisheni cha Azam.
Amesema zuio la kufanya mikutano liko kinyume na sheria iliyoanzisha vyama vya siasa.
“Jambo
jingine ambalo ni gumu zaidi, nikisema leo si mwana CCM sitaki kwenda
CCM, CUF wala Chadema, kwa utaratibu ulipo sasa siwezi kuanzisha chama
kwani huwezi kufanya mkutano wowote kwa sababu tunafunga kabisa mtu
kuanzisha chama,” amesema Sumaye na kuongeza,
“…,
CCM wao wanaonekana hawana wa kuwazuia, Mwenyekiti wao (Rais John
Magufuli) anakwenda popote, wakati wowote ingawa unashindwa
kumtofautisha na ziara za kiserikali.”
Kuhusu
hamahama ya wanachama amesema, “ “Wanacheza na fedha za wananchi,
mfano mbunge wa Kinondoni (Maulid Mtulia aliyehamia CCM) alikuwa CUF,
anakwenda CCM halafu wanamrudisha tena kugombea.”
“Sawa na yule wa Siha (Dk Godwin Mollel amehamia CCM) naye karejeshwa kugombea. Hii ni sawa na kuwatukana watu.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )