Askari wa vikosi vya ulinzi na usalama leo asubuhi Oktoba 20, 2018 wameonekana wakikagua na kuchukua vielelezo katika gari inayodaiwa kutumika kumteka mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’.
Gari hiyo aina ya Toyota Surf yenye namba T314AXX imetelekezwa katika barabara ya Ohio karibu na lango kuu la kuingilia viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni saa chache baada ya mfanyabiashara huyo kutupwa na watekaji katika viwanja hivyo.
Kufuatia kuonekana kwa gari hilo, barabara hiyo imefungwa.
Jana, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro alizungumza na waandishi wa habari na kuonyesha picha ya gari hilo, akieleza kuwa lilitumiwa na watekaji.
Hata hivyo, jana katika picha hizo gari hilo lilikuwa na namba AGX 404 MC.
Magari saba ya polisi yameegeshwa kando ya barabara hiyo huku askari wakiendelea na uchunguzi.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )