Waswahili wanasema ahadi ni deni.. akina
dada ambao wanafanya biashara ya kuuza miili yao Nigeria nao wanaahidi
kutimiza ahadi yao ya kutoa huduma bure kwa wateja wao nchi nzima.
Chama cha wasichana hao ambao
wanafanya biashara hiyo Nigeria waliahidi kwamba wako tayari kutoa
huduma bure kwa mtu yoyote iwapo Rais Buhari atashinda Uchaguzi huo.. Kwa kuwa tayari Buhari
kashinda wamesema watatoa huduma hiyo kwa siku tatu bure iwapo Rais
huyo ataruhusu biashara hiyo kuwa halali kabisa kama ilivyo biashara
nyingine.
Chama hicho ambacho kinaitwa NANP
kimesema iwapo biashara hiyo ikihalalishwa itasaidia waweze kufanya
biashara yao kwenye mazingira ya usalama zaidi hata wa afya zao.. NANP
walikuwa na imani kwamba Rais Buhari ataruhusu biashara hiyo japo mpaka sasa hajatoa taarifa yoyote.
Iliwahi kusikika pia kutoka Kenya ambapo
wanawake wanaofanya biashara hiyo waliandamana mpaka kwa Mwanasheria
Mkuu kutaka biashara yao ihalalishwe, watambulike na walipe kodi kama
wafanyabiashara wengine tu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )