Mtanzania mmoja ambaye
alikamatwa kuhusiana na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha
Garissa, Kenya (jina linahifadhiwa) ahojiwa.
Taarifa zilizopatikana juzi usiku na kutangazwa na Shirika la Utangazaji
la Uingereza (BBC), zilieleza kuwa Mtanzania huyo alihojiwa kuwapo
kwake katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba siyo mwanafunzi wala
mtumishi katika chuo hicho.
Taarifa hizo zinasema kuwa Mtanzania huyo ni miongoni mwa watu wanne
waliokuwa wamejificha katika mabweni ya chuo hicho na kati yao, wawili
walibainika kuwa ni wanafunzi.
Baada ya kuhojiwa akakiri kuwa wamepanga kufanya shambulio kubwa nchini
Tanzania katika Tamasha la Pasaka lilopangwa kufanyika tarehe 05/04/2015
Dar es salaam.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alipoulizwa jana
kuhusu Mtanzania huyo,alikiri hayo na kusema bado wamemuweka chini ya
ulinzi kwa ajili ya uchunguzi zaid
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )