BABA wa
marehemu mwigizaji Steven Kanumba, Charles Kanumba, amemuumbua mwanamke
aliyezaa naye staa huyo, Flora Mtegoha kwa kitendo chake cha kufuatilia
maisha ya msichana aliyewahi kuwa mpenzi wa mtoto wao, Elizabeth
Michael ‘Lulu’.
Akizungumza kwa njia ya simu mwanzoni
mwa wiki hii, mzee huyo anayeishi Shinyanga, aliliambia gazeti hili kuwa
ni jambo la kutia aibu kuona mzazi mwenzake akimlaumu Lulu wakati
ukweli ni kuwa hakuwahi kuwa mke wala kuzaa na marehemu mtoto wao.
“Mzazi mwenzangu amekosea, Lulu hakuwa
ameolewa wala kuzaa na Kanumba, siyo ukoo wake wala wa Mtegoha, kwa nini
anamlalamikia? Amuache awe huru na maisha yake.“Lulu kama binti
anatakiwa kuwa huru kwa kutayarisha maisha yake, mimi namuunga mkono
Lulu na kumbariki katika maisha yake,” alisema mzee Kanumba.
Wiki kadhaa zilizopita, Mama Kanumba
aliripotiwa kufanya misa ya kumbukumbu ya kifo cha mwanaye, lakini
akatoa maneno makali kutokana na msichana huyo kushindwa kuhudhuria
katika shughuli hiyo.
Ilidaiwa kuwa mama huyo alisema Lulu
ameacha kuwa karibu naye tofauti na zamani ambako alikuwa akimjali na
kumthamini, kitendo ambacho kilienda sambamba na kutoelewana kati yake
na mama mzazi wa msichana huyo muigizaji.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )