KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida waumini wa dini ya kiislamu pamoja na viongozi wa dini hiyo wilaya na mkoa wa Geita, wameandamana mpaka kwenye familia ya marehemu Samweli Malugala wakitaka kufukua mwili wake uliozikwa kikristu na ndugu zake.
Sakata hilo limekuja siku moja baada ya kuzikwa nyumbani kwao katika mtaa wa Mkolani kata ya Nyankumbu mjini Geita, ambapo viongozi wa dini ya Kiislamu walifika nyumbani kwa marehemu kutoa zuio la kuzikwa, na kwa vile hawakuwa na vigezo hawakuweza kufanikiwa kusudio lao.
Jana majira ya saa sita mchana Waislamu wakiwa wameongozana na maimamu wa msikiti wa ijumaa mjini Geita pamoja na mwenyekiti wa bakwata Mtaa wa Kalangalala walifika mpaka kwenye familia ya marehemu Samweli na hapa na kuanza kuongea kilichowapeleka.
Naye mwanafamilia Lucas Paul ambaye ni mtemi wa sungusungu Mtaa wa Mkolani , amewataka wafuate taratibu ya kufanya zoezi lao wakiwa chini ya uongozi wa Mtaa au Kata.
Muda mfupi baada ya malumbano hayo, mkuu wa polisi wilaya ya Geita Ali kitumbo amefika katika enao hilo la tukio na kuwataka Waislamu wafuate taratibu na kwamba wao polisi wako tayari kusimamia zoezi hilo.
Pamoja na kwamba marehemu amekwisha zikwa kikristu kesi ya msingi itaanza kusikilzwa tarehe moja mwezi machi mwaka huu katika mahakama ya wilaya ya Geita, ambapo itaamua nani ana uhalali wa kuuzika mwili huo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )