Ni ukweli kuwa Diamond na Alikiba ni wasanii ambao hawapatani kwa muda mrefu.
Kutokana na ugomvi wao uliopo umepelekea
mpaka mashabiki wao kuanzisha team, team hizi zinakuwa zinamsupport
msanii wao na kumpinga mpinzani wao.
Diamond aliwahi kuhojiwa kwenye kipindi
cha Sporah Show alisema, “Kuna wimbo wa Alikiba ‘Singel Boy’ nilimuomba
Alikiba kuingiza sauti tulipokuwa studio alikataa na kusema kuwa nataka
mteremko.”
Alikiba aliwahi kusema, “Kwenye wimbo wa
‘Lala Salama’ niliingiza sauti yangu lakini nilishangaa kuona sauti
yangu imefutwa kwenye wimbo huo, kibaya zaidi ametumia melody yangu
niliyorekodia mwanzo.”
Hakuna mwenye uhakika wa hili kuwa nani
ni mkweli na nani anatudanganya. Ugomvi wao unazidi kuwa mkubwa kila
siku, sasa hivi umeenda mbali zaidi mpaka msanii atakayekuwa karibu na
mmoja kati ya hawa wawili wenye ugomvi mwingine anakuwa anachukia.
Ukiwa karibu na msanii mmoja unakosa
support ya upande wa pili, hata kama umeingia kwenye mashindano hutaweza
kupigiwa kura na mashabiki wa team nyingine. Hili linarudisha nyuma
muziki wetu Angalia kilichotokea kwa Ommy Dimpoz hutataka kuangalia tena
nyuma, unakumbuka Wema Sepetu mwanzo alikuwa team gani na sasa yuko
wapi? Vipi Jokate kilichomtokea kwenye pande zote mbili kwa sasa
unadhani atakuwa wapi tena?
Angalia support wanayopeana Wanigeria
kwenye tuzo na muziki wao, hawaonyeshi tofauti zao japo wapo wengi
hawapatani. Kwanini tugombee fito wakati tunajenga nyumba moja? Ni
ukweli usihitaji ushahidi, Diamond akiingia kwenye tuzo zozote mashabiki
wa Alikiba hawampigii kura wanaona ni bora kumpigia kura msanii wa nje
ili Diamond akose hiyo tuzo.
Hilo pia lipo kwa upande wa pili kama
Alikiba akiingia kwenye mashabiki wa Diamond hawampigii kura. Hata kama
Wizkid ana ugomvi na Davido mashabiki wao hawawezi kumpigia kura Diamond
au Alikiba ili ashinde tuzo.
Kuna haja wa kuweka tofauti pembeni na
kuhakikisha muziki wetu unafika mbali zaidi, ‘Kidole kimoja hakivunji
chawa’, unajisikiaje tunaposhiriki kwenye tuzo za nje kwenye category
moja unawaona wapo wasanii wanne kutoka Nigeria na mmoja tu ndiyo wa
Tanzania.
Utajisikiaje siku ukiona Jay Z akapenda
kufanya kazi na msanii wa Tanzania? Kwa hili lililopo sasa hivi kufika
huko ni mbali sana, kila team inafanya msanii mwingine asifanikiwa.
‘Adui muombee njaa’, kwetu imekuwa tofauti tunaombeana wenyewe hiyo
njaa.
Bongo5
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )