Ipo wazi Diamond
anamchango mkubwa kwenye tabia za wasanii waliochini ya label yake ya
WCB, ni ngumu kukutana na Diamond Club kama hafanyi show, ndio sababu
kubwa huwezi pia kukutana na wasanii waliochini ya label hiyo viwanjani .
“Labda nizungumze kitu kimoja, WCB sio
mimi tu hata wasanii wengine ambao watatoka WCB kuna life style ambayo
watafuata, lakini mimi kama mimi sipajui club kabisa, sijawahi kwenda
club sitokagi,” amefunguka Harmonize.
Mbali ya kuwa boss wao mwenyewe sio mtu
wa viwanja, Harmonize amesema Diamond amewatengenezea mazingira ya
kupenda kukaa maeneo ya studio,
“Pale ofisini kuna studio mle mle
ndani, kuna vyumba ambavyo ukirekodi ukichoka unakaa unarefresh mind,
kuna game station mnakaa mnacheza game, alafu pia kuna vyumba vya kuishi
mule mule, muda wenyewe wa kutoka unakosa, alafu pia ukizingatia CEO
mwenyewe wa WCB hana hizo mambo za kwenda club, so sisi tunajifunza
kupitia yeye,” alisema Harmonize.
Harmonize pia amedai kuwa hawapendi kujichanganya ili kukwepa skendo zisizo na maana.
Source: EATV
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )