Featured
Loading...

Mwanamuziki Malaika Amefunguka Kuhusu Tetesi za Kuhongwa Gari Aina ya Ranger Rover.///


STAA wa Ngoma ya Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’ kwa mara ya kwanza amefungukia gari jipya la kifahari analodaiwa kumiliki aina ya Range Rover Sport kuwa hajahongwa kama watu wasemavyo.

Akichonga na Showbiz, Malaika aliyewahi kubamba pia na Ngoma ya Sare Sare na Mwamtumu alisema kuwa katika picha ambayo aliachia kwenye ukurasa wake wa Instagram hivi karibuni ni kweli gari lake na kwamba hajahongwa na mtu.

“Ni kweli lile gari ni la kwangu na nipo katika utaratibu wa kulishughulikia litoke bandarini, sijahongwa na mtu jamani hao wanasema tu ila mimi nimesema nilichosema inatosha,” alisema Malaika.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top