Hii
ni aibu yao! Picha zinazomuonesha staa wa Hip Hop anayetamba na ngoma ya
Shika Adabu Yako, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa katika pozi
la nusu utupu na msanii wa Bongo Fleva, Aisha Nyange ‘Dayna’ zimevuja
pasipo wenyewe kujua.
Katika
baadhi ya picha hizo, Nay anaonekana akiwa amemkumbatia Dyna huku
wakiwa hawana nguo za juu, yaani Nay hana vesti wala tisheti na hata
Dyna akiwa hana nguo yoyote ya kumstiri juu.
Baada ya kuzidaka picha hizo gazeti hili
lilivuta waya na kuwatafuta wahusika ambapo baada ya kumpata Nay na
kumdadisi kama anabanjuka kimalovee na mwanadada huyo alikuwa na haya ya
kusema;
“Dah, hapana bwana, hizo picha
hatukupanga zitoke. Kuna ambazo zilipitiliza si unajua wakati wa kupiga
studio zipo ambazo huwa hamzitumii sasa sijui nani alizivujisha hizo
mbaya.”
Baada ya kumalizana na Nay, Dyna naye
alitafutwa ili kuifungukia ishu hii, ambapo baada ya kupatikana alidai
zilikuwa ni picha za kwenye kava la ngoma yake ya Nitulize
aliyomshirikisha Nay lakini alipoulizwa kuhusu zile zilizovuka maadili,
alijibu:
“Aah! Hilo ni suala binafsi, lakini
naomba iishie kufahamika kuwa Nay ni mtu wangu wa karibu lakini hatuna
uhusiano wa kimapenzi, ilikuwa ishu ya kazi tu.”
-GPL
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )