Featured
Loading...

Ndoa ya Rayuu Chali Baada ya Wiki Moja Tu..Kisa Skendo Chafu za Magazetu


Baada ya kutamba kuwa tayari amepata mume wa maisha, mambo yameharibika msanii wa filamu Rayuu, kwani sasa hatoki nje wale hapokei simu za shoga zake.

Wiki moja iliyopita msanii huyo aliiteka mitandao ya kijamii hasa instagram, kwa picha zake za harusi huku akiwa na bwana ake ambaye sasa si bwana tena.

Chanzo kikubwa cha kuvunjika kwa ndoa hiyo inadaiwa kuwa mwanaume ambaye alimuoa ni mume wa mtu, ambaye tayari mke wake ana ujauzito wa miezi mitatu, lakini pia inadaiwa kuwa ni kutokana na matukio kadhaa ya msanii huyo.

Rayuu alitafutwa ili kujibu tuhuma za kuachika, alijibu yote ni matokeo na kuachika kwake isiwe sababu ya yeye kusemwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Sina muda wa kuzungumzia mambo hayo kwani nilipofunga ndoa sikusema, sitaki nasema sitaki, maana watu wanaona ni jambo la kuzungumzwa mbona wapo wanaoolewa kifahari na wanaachika,” alisema kwa ukali kisha akakata simu

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top